Mwanzo > Habari > Content

Nyaraka mbili za BFSU Zaorodheshwa katika Matunda Yaliyopatikana Kupitia Mazungumzo ya Marais wa China na Urusi

Updated: 2026-05-20

Tarehe 20 Mei, Rais wa China Mhe. Xi Jinping na Rais wa Urusi Mhe. Vladimir Putin walizindua kwa pamoja “Mwaka wa Elimu baina ya China na Urusi” utakaoendelea kwa miaka miwili. Mkuu wa BFSU Prof. Jia Wenjian alialikwa kuhudhuria ufunguzi.

Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Wananchi cha Urusi katika Sekta ya Lugha ya Kirusi na Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing na Idara ya Mambo ya Vijana ya Urusi katika Sekta za Elimu na Sera za Vijana yameorodheshwa katika orodha ya matunda yaliyopatikana kupitia mazungumzo ya marais wa China na Urusi.

Baidu
map